Timu ya soka ya waandishi wa habar iza michezo nchini (Taswa FC) siku ya sikukuu ya Pasaka itashiriki katika tamasha la mpira wa miguu lililopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Tabata Shule ya Msingi.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa timu zaidi ya nane zitashirikiki katika bonanza hilo na timu yake imejidhatiti kuibuka na ushindi.
Majuto alisema kuwa wanachukulia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya safari yao ya Arusha na mechi ya kuiaga sikukuu ya Pasaka kwani Jumatatu ya Pasaka watapambana na timu ya wauza maua kutoka Arusha.
Alisema kuwa wageni wao wanatarajia kuwasili jijini siku ya Pasaka na baada ya kusheherekea na wakazi wa Dar es Salaam, watacheza mechi hiyo ambayo itashirikisha pia timu ya Taswa ya Netball maarufu kwa jina la Taswa Queens.
Michezo yote hiyo inatarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii au Kinesi kwa kutegemea nafasi ya viwanja hivyo.
No comments:
Post a Comment