Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Jan Poulsen ametangaza majina ya wachezaji 23 ambao wataiwakilisha Tanzania kwenye mechi ya AFCON dhidi ya Jamhuri ya Kati hapo Machi 27 kwenye uwanja wa Taifa.
Katika uteuzi huo, Yanga na Azam zina juma ya wachezaji wanne kila mmoja wakati Wekundu wa Msimbazi, Simba ina watatu huku Mtibwa Sugar, JKT Ruvu na ST Long An ya Vietnam zina wachezaji wawili wawili.
Timu hiyo itaingia kambini Machi 17 kwenye hotel ya Atrium ya Sinza bila ya wachezaji wa Simba ambao wanajiandaa na mechi dhidi ya TP Mazembe. Simba SC inatarajia kuondoka Jumamosi kwenda Lubumbashi, DR Congo kwa ajili ya mchezo huo uliopangwa kupigwa Machi 20.
Wachezaji wa timu hiyo wanatarajia kujiunga na kambi hiyo siku ya Jumatatu, mara baada ya kurejea kutoka Lubumbashi.
KIKOSI KAMILI CHA WACHEZAJI WA STARS NI HAWA HAPA
MAKIPA
Shabani Kado (Mtibwa Sugar), Juma Kaseja (Simba) and Shaaban Dihile (JKT Ruvu).
MABEKI
Shadrack Nsajigwa (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Stephano Mwasika (Yanga), Haruna Shamte (Simba), Juma Nyoso (Simba) and Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya).
WACHEZAJI VIUNGO:
Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Jabir Aziz (Azam), Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mwinyi Kazimoto (JKT Ruvu).
WASHAMBULIAJI:
Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngasa (Azam), Mohamed Banka (Simba), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), John Bocco (Azam) and Mbwana Samata (Simba).
No comments:
Post a Comment