Timu ya soka ya Taifa ya umri chini ya miaka 23 itacheza mechi mbili za kirafiki kabla ya kupambana na Cameroon katika mchezo wa kufuzu wa michuano ya Olimpiki uliopangwa kufanyika Machi 26 mjini Younde, Cameroon.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelu alisema kuwa mechi hizo mbili zinaweza kufanyika hapa nchini au katika nchi hizo. Kihwelu ambaye ni maarufu kwa jina la Julio, alisema kuwa kwa sasa wapo kambini, Bamba Beach wakijiandaa na mazoezi ya mchujo kabla ya kupambana na timu hizo mbili.
Alisema kuwa timu yao ina wachezaji 44 na Machi 8 watachuja wachezaji hao kubakia 25 ambao watacheza mechi dhidi ya Msumbiji, Uganda kabla ya kupanda ndege kwenda Cameroon.
"Ni matarajio yetu kuwa tutafanya vrema katika mechi hizo zote tatu, naamini wachezaji wangu wana kila kitu na wanatambua majukumu yao," alisema Kihwelu.
No comments:
Post a Comment