Monday, March 14, 2011

HASIRA ZA TASWA FC ZAMALIZIKIA KWA PREMIER BINGO FC: YAICHAPA 9-2

HASIRA za timu ya Taswa FC za kufungwa mabao 3-0 na timu ya Kombaini ya Polisi Jamii zimemalizikia kwa timu ya wafanyakazi wa michezo wa bahati nasibu ya Premier Bingo betting FC baada ya kuichapa kwa mabao 9-2 katika mchezo maalum.

Mchezo huouliofanyika kwenye uwanja wa Ustawi wa Jamii ulikuwa mkali na wa kusisimua ambapo Premie Bingo FC ilitawala dakika 10 za mwanzo na kumfanya kipa wa Taswa FC Steven Mduma kufanya kazi ya ziada.

Ikiongozwa na mwenyekiti wake, Majuto “Ronaldo De Lima” Omary, Taswa FC ilipata bao la kwanza katika dakika ya 13 kupitia kwa Majuto kwa shuti la mbali.

Bao hilo liwachanganya sana Premier Bingo FC na kukutwa wakipchapwa bao la pili kupitia kwa Said Seif kufuatia pande safi la Majuto.

Premier Bingo FC ilijitahidi kutafuta bao, lakini ngome ya Taswa Fc chini ya Sweetbert Lukonge, Mohamed Akida, Juma Ramadhani na Fred Mweta iliondoa hatari zote.

Majuto alifunga mabao mengine mawili katika dakika ya 23 na 33 na kukamilisha hat-trick kabla ya Mohamed Abdallah kufunga la tano katika dakika ya 43 ya mchezo.

Premier Bingo ilianza kipindi cha pili kwa kufanya mabadiliko ambapo Mabago Kwezi aliingia upande wa kipa. Hata hivyo, kipa huyo alijikuta akifungwa mabao manne katika kipindi hicho.

Said Seif alifunga katika dakika ya 53 kufutia kazi nzuri ya Majuto kutoka wingi ya kushoro kabla ya Mohamed Abdallah kufunga mawili katika dakika ya 63 na 73 huku Juma Ramadhan akifunga bao la tisa.

No comments: