Thursday, March 3, 2011

WATATU SIMBA KUIKOSA YANGA JUMAMOSI

Jumla ya wachezaji watatu wa klabu ya Simba watakaa jukwaani Jumamosi wakati wenzao watapopambana na Yanga kwenye uwanja wa Taifa.

Wachezaji hao ni Mkenya, Hillary Echesa na wachezaji wawili kutoka Uganda, mshambuliaji Emmanuel Okwi na mlinzi, Joseph Owino.

Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Patrick Phiri alisema jana kuwa Okwi pamoja na kuanza mazoezi madogo madogo, bado hali yake si nzuri na stamala yake haitamwezesha kucheza mchezo huo kwa asilimia 100.

"Ndiyo kwanza ameanza mazoezi Jumatano, sidhani kama ataweza kupambana katika mchezo huo ambao ni moto wa kuotea mbali na una ushindani mkubwa, Echessa na Owino wao hawatakuwa katika bechi la wachezaji wa akiba na watakuwa jukwaani," alisema Phiri.

Kocha huyo raia wa Zambia aliwatoa wasiwasi wanachama, wapenzi na wadau wa timu hiyo kwani anaamni wachezaji waliobaki katika kikosi hicho watafanya vyema na kunyakua pointi zote tatu.

No comments: