Friday, March 18, 2011

'NCHIMBI AWAPONGEZA MABONDIA'

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi,
amepongeza uteuzi wa mabondia wa timu ya Taifa uliofanywa na
Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT).

Mwanzoni mwa wiki hii, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, alitangaza
kikosi cha mabondia 28 waliochaguliwa kuunda kikosi hicho ambacho
kitakuwa chini ya Kocha Mkuu Hurtado Pimenter kutoka Cuba na makocha
wazawa Benjamin Mwangata, Makoye Isangula na Edward Emanuel.

Dkt. Nchimbi alitoa pongezi hizo Dar es Salaam juzi katika kikao
chake na wajumbe wa Kamati ya Utendaji BFT, alipokutana nao kwa mara
ya kwanza tangu achaguliwe katika nafasi hiyo.

“Timu za Taifa zichaguliwe mapema kwani zinapochaguliwa karibu na
mashindano, wachezaji wetu hawapati maandalizi ya kutosha kwani lengo
la serikali ni kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya michezo,”
alisema Nchimbi.

Aliongeza kuwa, taswila la mchezo wa ngumi ilianza kupotea nchini
kutokana na kashfa ya dawa za kulevya iliyotokea katika uongozi wa
Alhaj Shaaban Mintanga hivyo jukumu la uongozi wa sasa ni kutafisha
taswila hiyo katika jamii.

Alisema umefika wakati wa BFT, kuimarisha mfumo wa mawasiliano katika
ngazi za chini na kuboresha utendaji kazi ili kupata mabondia wenye
vipaji na uwezo wa kuitangaza Tanzania kimataifa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, alisema jitihada
kubwa zilizoanza kufanywa na shirikisho hilo ni kuhakikisha mabondia
wote, wanaingia katika mpango wa Polisi Jamii ili wahusika wa biashara
hiyo na watumiaji, waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya
sheria.

No comments: