Thursday, March 3, 2011

TASWA FC YAALIKWA TENA ZANZIBAR

Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC imealikwa tena Zanzibar kushiriki katika mchezo maalum wa kuzindua timu ya wana habari wa huko, Zaswa FC. Safari hiyo ya Taswa FC itafanyika mwezi ujao kabla ya sikukuu ya Muungano.

Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary amewataka wachezaji wa timu hiyo kufanya mazoezi zaidi ili kwenda kuonyesha kandanda safi na kuweka rekodi ya kutofungwa huko Tanzania Visiwani na mwaka huu kwa ujumla.

Majuto alisema taarifa kamili na utaratibu wa safari hiyo utatolewa hapo baadaye.

No comments: