Tuesday, March 15, 2011

YANGA, JKT ZAINGIZA MIL 19/-

Mechi namba 113 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa Machi 12 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam imeingiza sh. 19,475,000. Baada ya kulipa asilimia 18 kwa Serikali ambayo ni sh. 2,970,763 ikiwa ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na gharama za awali za mchezo sh. 3,639,600 fedha zilizobaki kwa ajili ya mgawanyo ni sh. 12,864,637.

Katika mgawanyo huo kila timu ilipata mgawo wa sh. 3,859,391. Mgawo mwingine ulikwenda kwa gharama ya mchezo (sh. 1,286,464), Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania- TFF (sh. 1,286,464), Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF (sh. 643,232), Uwanja (sh. 1,286,464), Baraza la Michezo la Taifa- BMT (sh. 128,646) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam- DRFA (sh. 514,585).

Watazamaji 4,028 walilipa kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 15,000, sh. 8,000, sh. 5,000 na sh. 3,000.

Nayo mechi ya ligi hiyo kati ya Azam na Mtibwa Sugar iliyochezwa Machi 13 mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kushuhudiwa na watazamaji 1,021 iliingiza sh. 3,718,000. VAT kwa mechi hiyo namba 114 ambayo kiingilio kilikuwa sh. 5,000, sh. 3,000 na sh. 2,000 ilikuwa sh. 567,153.

Baada ya kuondoa gharama za awali za mechi mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh. 468,494, gharama ya mchezo (sh. 156,165), Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania- TFF (sh. 156,165), Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF (sh. 78,082), Uwanja (sh. 156,165), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam- DRFA (sh. 62,466) na Baraza la Michezo la Taifa- BMT (sh. 15,616.

No comments: